Friday, August 24, 2012

MUME NA MKE....


Mke alikwenda kulalamika kwa mumewe kuwa kuna jamaa mgeni jirani yao kamtukana kuwa ana mdomo kama tairi la trekta...

Daaah, mume akapandisha na kuapa kutoa adhabu kali sana atakapokutana na huyo mshenzi, yani atamtembezea kichapo mpaka ajute!!! 

Siku walipokutana na huyo jamaa mume kanywea maana jamaa alikuwa baunsa wa ukweli;
MUME: "Mambo jirani?!?"
JIRANI: "Poa tu niambie..."

MUME: "Aaaaah, Swaaaari.... Daaaaah, jirani nasikia ulimtukana mke wangu kuwa ana mdomo kama tairi la trekta..."
JIRANI: "Ndio, kwani vipi...?!?"

MUME: "Aaaaaah, tairi la mbele au la nyuma?!?"
JIRANI: "La nyuma...."

MUME: "Ah, jirani bwana, mi nilidhani ulisema la mbele, inaonekana mimi na wewe tunawaza sawa, ila tu sijamwambia wife, si unajua akina mama wanavyoweza kupaniki, nashukuru kwa kumchana live!!!!"

No comments:

Post a Comment