Dogo alikuwa kwenye gari na baba yake wakitoka harusini walipocmamashwa na trafic..
Trafic: "Hivi unajua taa yako moja ya kushoto haiwaki?!"
Dingi: "Daaah, nisamehe mkuu, nlikuwa cjui kabisa, itakuwa imeungua muda si mrefu.."
Dogo: "Lakini baba c toka juzi nakwambia uibadilishe taa ya gari imeungua huckii?!"
(dingi akamcheki kwa hacra then akachuna..)
Trafic: "Embu toa leseni yako..."
Dingi akampa leseni trafic...
Trafic: "Mbona leseni yako ime-expire miezi mitatu iliyopita?!"
Dingi: "Samahani afande.. Ntaenda renew kesho.."
Dogo: "Lakini baba... mama c alisema hiyo leseni ni feki inabidi uombe mpya?!"
Dingi: "We mbwa unajua nitakukata makofi wewe?! Embu funga bakuli lako..."
Trafic: "Hivi we mtoto baba yako cku zote anaongeaga na wewe hivi nyumbani?!"
Dogo: "Hapana... Huwa anakuwa hivi akishakunywa sana pombe na kuwa TILALILA!!!"
No comments:
Post a Comment