Thursday, January 26, 2012

SHAROBARO

Kuna Sharobaro mmoja alibahatika kwenda kusoma majuu kwa miaka minne....

Aliporudi TZ, mwendo wake ukawa wa kudunda dunda na kuinamia upande mmoja (kushoto) huku bega la kulia akiliinua...

Siku moja mama yake akamuuliza...
"Hivi we mtoto kwa nini unatembea ukiwa umebend upande mmoja?!? Ulipata ulemavu huko?!?"

Jamaa akamjibu...
"Aah, mother unajua nnilipokuwa majuu muda mwingi nikienda class nilikuwa nashika mavitabu kwa kutumia mkono wa kushoto hivyo nshazoea bi mkubwa au sio?! Ka vipi nikaushie, usimind wala nini...."

Mama yake akamkatisha...
"Pumbavu!!!!! Nyamaza mshenzi mkubwa wewe... Mbona mimi nimewazaa nyinyi kumi na mbili lakini nikitembea mbona sikatikati viuno?!?!"

No comments:

Post a Comment