Sunday, January 29, 2012

JAMAA NA SIMBA


Kulikuwa na jamaa mmoja mkali sana wa kucheza na simba kwenye maonyesho ya sarakasi... Siku moja alikuwa amekaa na rafiki yake wakibadilishana mawazo... Rafiki yake akaanza kumuuliza maswal ya kizushi...

Rafiki: "Hivi kwa mfano simba akaangusha ile stuli ndefu unayoitumiaga akiwa chini utafanyaje?!"

Jamaa: "Ntampiga na ile fimbo ndefu nayokuwaga nayo..."
Rafiki: "Fimbo ikivunjika je?!"

Jamaa: "Ntashikilia kamba juu bila kushuka..."
Rafiki: "Kamba ikikatika!?"

Jamaa: "Ntampiga na mjeredi naomchapaga nao..."
Rafik: "Mjeledi akiung'ata na kuuvuta!?"

Jamaa: "Ntampiga na viti..."
Rafiki: "Kama akikwepa viti itakuwaje?!"

Jamaa: "Ntawaomba walinzi wampige risasi..."
Rafiki: "Kama risasi zikimkosa?!"

Jamaa: "Ntaamua kukimbia..."
Rafiki: "Kama ukikosa pa kukimblia??!"

Jamaa: "Ntampiga na 'kinyesi' mpaka akimbie yeye..."
Rafiki: "Ukikosa hicho KINYESI????!?"

Jamaa: "We bwege nini?! Hivi huyo SIMBA aangushe stuli, akate kamba, ang'ate mjered, avunje fimbo, akwepe mshale, risas zimkose, nitakosa mavi ya kutosha kwenye suruali yangu ya kumpiga nayo????!"
 ·  ·  · December 29, 2011 at 2:43am near Dar e

No comments:

Post a Comment