Thursday, January 26, 2012

Mafather outing...

Mafaza wawili wa kikatoliki walikwenda kula bata visiwa fulani vya starehe, ili wasishitukiwe wakaamua kuingia duka moja na kuchagua swaga za kipededjee wakatupia hadi bichi, kidogo akakatisha demu mmoja kavaa kibikini kdogo sana wale mapadre wakammezea mate wakamtolea mijicho. Basi yule demu akawasalimu mmojammoja, Shikamoo faza. wakashangaa katujueje. Kesho yake wakabadili swaga demu yule akawasalimu tena vilevile. wakaamua kumuuliza amewajuaje. Demu akajibu inamaana mmenisahau mi ni Sista Scola. 

No comments:

Post a Comment