Mwanamke mmoja alikuwa na tatizo la mlango wa kabati chumbani kwake ambao kila mara gari kubwa likipita nje huwa mlango unafunguka...
Basi kutokana na tatizo hilo akaamua kumuita fundi aje kurekebisha...
Fundi ambaye kidogo alikuwa na kigugumizi akamwambia kabla, hajatengeneza inabidi acheki ili ajue kwanza tatizo... Kwa hiyo jamaa akaamua kuingia ndani ya kabati halafu akamwambia afunge ili aone kinacho fanya lijifungue kila gari likipita... Ila kabla hajaingia kabatini akaomba avue shati lake jeupe ili licchafuke..
Ile anafunga tu, mume wa yule mwanamke aliyekuwa kambini jeshini kwa muda mrefu sana akaingia...
Mke kwa mshangao na furaha ya kumuona mumewe ambaye alikuwa safarini cku nyingi akazimia...
Jamaa kumsogelea mkewe akasikia kabati linacheza cheza kwa ndani... Kufungua akamkuta yuke fundi...
Mume: "Shiiiiit?! Aroooo, unafanya nn ndani kwangu?!"
Fundi akajibu huku kijasho kikimtoka:-
"Sa, sa, sa sa samahaaaani mkuuu... Kiukwe kwe kwe kweeeli tu, tu, tu tu tu msubiiiiiri tu kwa kwa kwaaanza m, m, m, mmmkeeeo a a a ammmke kwa kwa kwa kwasabaaabu huta ni ni nieeleeewa... Ila ni ni ni niilikuuuwa na na na nasubiiiiiri ga ga ga gaaari kubwa li li li liipiiiiiite...!!!"
No comments:
Post a Comment