Saturday, January 28, 2012

MLEVI BAR

Mlevi kaingia bar na kumwambia meneja....

"Ebwana daaaah... Unajua mi ninashabaha ile mbaya... Naweza kujaza mkojo kwenye ileeee chupa ya juu kabisa counter bila hata kudondosha hata tonye..."

Meneja akabisha na kupinga kabisaaaa, mshikaji akamwambia....
"Basi tufanye hivi... Nakupe laki moja nikidondosha hata tonye pembeni, na nikishindwa we nipe bia 3 tu..."

Meneja akaona isiwe tabu, kucheki huku na kule akaona baa watu wako busy busy akakubali...

Bila taabu, jamaa akasogea kaunta.... Akaanza kukojoa lakini hakufikisha hata punje kwenye chupa....

Meneja akadai chake, mshikaji akatoka njee na kurudi na kama milioni moja mkononi huku akitabasamu... Akampatio meneja pesa yake...

Kwa mshangao meneja akauliza...
"Hiyo mihela umeokota wapi na mbona unatoa kirahisi hivyo huku ukitabasamu???!!"

Jamaa akamwambia....
"Nimeweka dau la laki moja moja na watu kama kumi na wale jamaa paleee nje wanaochungulia dirishani kuwa naweza kuja kukojoa kaunta na ucnifanye chochote!!!"

No comments:

Post a Comment