Sunday, January 29, 2012

MASKINI JEURI

‎"Nimechoka!!!! Yani mimi ndo kila cku nakosa rizki kwa Mungu?!" Alilalamika baba mmoja huku amejiinamia chini ya mti wa mbuyu akiwaza..

Akaendelea kusema... 
"Kama hutaki niishi duniani, niangushie huu mbuyu nife tu, sioni raha ya maisha.."

Ghafla pande moja la mti likaanguka kumuelekea pande alipo...

Duuh, jamaa akaondoka mbio huku akilalamika..
"Nakuomba rizki kila cku hunipi, leo nakutania kufa ata dakika haijaisha.. Khaaa!! Hutaniwi?!"

No comments:

Post a Comment