Sunday, January 29, 2012

TARIMO NA MASAWE

Tarimo alikuwa anamdai Masawe nahivi ndivyo ilivyokuwa kwenye simu...
Tarimo: "Haloo.. Habari yako Masawe..."
Masawe: "Safi kabisa aiseee..."

Tarimo: " Vp, Kuhusu deni langu?!"
Masawe: "Sikusikii freshi... Unasema?!"

Tarimo: "Deni langu, vp?!"
Masawe: "Yani nakusikia kwa mbaaaaaaaaali!!!"

Tarimo: "Mechi ya jana ulicheki ya starz na Rwanda?!"
Masawe: "Ebwana... Taifa starz wanajitahidi sana siku hizi, yani..."

Tarimo: "Pesa yangu utanilipa lini?!"
Masawe: "Simu imeanza katika katika tena..."

Tarimo: "Deni langu utanilipa au?!"
Masawe: "Simu imeanza katika katika tena aisee... Naona hapa pembeni watoto wamewasha BOLINGO ndiyo maana simu inakatika nguja nizime... eheee?!"

Tarimo: "Pesa yangu VIPI?!"
Masawe: "Hapo ndiyo umetibua kabisa yaani hata sisikii kitu aisee!!"

Tarim: "Ninaweza kukupa ofa ya pombe leo?!"
Masawe: "Ewaaaah, hapo nmekusikia kuliko station yoyote hapa Tanzania... Yani na nilivyo na kiu ntashukuru sana aiseee..."

Tarimo: "Pumbavu sana, vingine unasikia.. Pesa yangu unalipa au hulipi?!
Masawe: (KIMYA)

Tarimo: "Haloo, haloooo, unanisikia?!"
Masawe: "SIMU YA MTEJA ULIYEKUWA UNAONGEA NAYE, HAIPATIKANI, TAFADHARI JARIBU KWANZA KUSAMEHE DENI... BEEEEEEEEEP!!!"

1 comment: