Sunday, January 29, 2012

Mapolisi wa usalama barabaran

Cicco alisimamishwa na mapolisi wa usalama barabarani Arusha akiwa na wenzake ndani ya 'Mercedes benz...'

Cicco: "Vp mkuu?! Kuna tatizo lolote mkuu??!"
Traffic: "Hapana, Ili nimepima uendeshaji wako mita 100 kabla hujafika, na nimeona ulikuwa unaendesha vizuri sana.. Hivyo mimi kama Afisa mkuu wa usalama barabarani nakuzawadia tuzo ya Dereva bora wa mwaka 2011..."
Cicco: ""Ebwana, daaah... Asante mkuu, ila ningefurahi zaidi kama ungenipa leseni badala ya hiyo tuzo yako..."

Traffic kabla hajauliza chochote kuhusu leseni.... Sherry aliyekuwa kwenye siti pembeni ya Cicco akaropoka...
"Afande usimsikilize huyo, hayo ndiyo matatizo yake ya kuropoka ropoka akiwa amelewa..."

Hassan aliyekuwa siti ya nyuma na washkaji wengine wawili akashtuka usingizini na kuropoka..
"...daaah ona sasa, mi nilisha waambie, tusinge fika mbali na gari la wizi, cheki sasa afande amesha tukamata..."

Kabla Hassan hajamaliza kuongea, Challe na Alloyce waliokuwa kwenye buti wakasikika wakigonga gonga buti huku wakipiga kelelee...
"Oyaaaaaa, mbona gari haliendi?! Hizi bunduki zinatuumiza huku na joto limezidi... Kama vipi njoeni mkae nyinyi si tuendeshe... Bado tu hatujavuka BORDER?!"

No comments:

Post a Comment