Sunday, February 12, 2012

BONGO TAMBARALE HATA WAMAREKANI NA WAJAPANI WAKO NYUMA

Mmarekani, Mjapani na Mtanzania walikutana chuo Kikuu cha Harvard wakaanza kutambiana kuhusu uchaguzi katika nchi zao. Mmarekani akajigamba kwa kusema sisi wamarekani tukishapiga kura, kura zinahesabiwa hapohapo na mashine na tunapata matokeo hapo hapo. Mjapani akajigamba akasema sisi kwetu huna haja ya kusubiri matokeo kwani unaenda nyumbani na tume ya uchaguzi inayatuma matokeo moja kwa moja katika computer yako. Mtanzania akasema mimi nisemeje sasa, Akawaambia yaani nyie mnachukua muda mrefu hivyo, yaani sisi hata kabla ya uchaguzi tunajua mshindi ni nani.

No comments:

Post a Comment