Sunday, February 12, 2012

JAMAA NA DOCTOR

Jamaa fulani alienda kwa doctor na kumwambia...
Jamaa: "Samahani doctor... Kichwa kinaniuma na ninamawazo sana... Hivi wewe ukiacha haya madawa huwa unafanya nini ili kutuliza maumivu?!?"
Doctor: "Aaaaaah, kwa mimi huwa nafanya mapenzi na mke wangu na nakuwa freshi kabisa..."

Wote wakacheka sana, jamaa akapewa dawa na kuondoka... 

Baada ya wiki 2 jamaa akarudi tena kwa doctor....
Doctor: "Vipi, unajisikiaje kwa sasa ndugu yangu..."
Jamaa akatabasamu na kujibu;
"Kweli ww ni Daktari bora sana na ulisema kweli... Najickia vizuri sana... Pia nyumba yako nzuri sana na mkeo kwa kweli anafaa sana kutuliza naumivu...!!!"

No comments:

Post a Comment