Sunday, February 12, 2012

hoteli moja ya KIMATAIFA

Jamaa fulani aliingia hoteli moja ya KIMATAIFA na alipofika ndani alifurahi sana baada ya kukuta kuna computer ya kutumia chumbani kwake, tena iliyounganishwa na Internet... Jamaa bila hata ya kupoteza muda akaamua kumwandikia e-mail mkewe.... Kwa bahati mbaya katika kutuma akakosea na kumtumia mwanamke mmoja mjane ambaye ndo alitoka kwenye mazishi ya mumewe...

Yule mwanamke aliyetoka kwenye mazishi, baada tu ya kufika kwake bila ya kupoteza muda akawasha laptop yake na kuanza kusoma e-mail zake ili aweze kujibu salamu za rambi rambi toka kwa ndugu, jamaa na marafiki...

Baada ya kusoma e-mail moja tu ya kwanza yule mama akapiga kelele na kuzimia....

Mwanaye wa kwanza wa kiume akatoka mbio mpaka chumbani na kumkuta mama yake kazimia, kucheki pembeni akaona kuna e-mail mamake alikuwa anaisoma, so jamaa akaamua kuipitia faster kujua kama ndio tatizo... E-mail ilikuwa hivi...

****************
To: My lovely wife!!!

Najua lazima unashtuka sana kupata hii e-mail toka kwangu...
Sikutegemea kukuta computer hupa ila zipo na tunaruhusiwa kuzitumia... Ndio nimefika huku na hapa ndo wamenipa chumba changu... Nimepokelewa vizuri sana tofauti na nilivyo tarajia... Watu wamejaa sana ila nafasi bado zipo na naona kila kitu kiko sawa na wamekuandalia vizuri na wewe sehemu ya kufikia.. Nakusubiri kwa hamu sana mke wangu na usiogope, safari ni fupi na utafika salama usijari, ukifika tu kuna watu maalumu watakupokea... Mwambie huyo mwanetu mkubwa wa kiume na wadogo zake wote watakuja jumuika nasi wiki ijayo hivyo wajiandae...

Nategemea sana ujio wako wa kesho ili tuwe wote pamoja.

Can't wait to see you honey, ♥ :)
From: Your lovely, Husband!!!

*****************************************

No comments:

Post a Comment