Wednesday, March 28, 2012

Michango ya kanisa

Michango ya kanisa ilikuwa inakusanywa
karibu na sanamu la Bwana Yesu. Teja
akasubiri mpaka watu wote wameondoka
akaenda kwenye sanamu akaanza kuongea
nalo, "Bwana Yesu nina shida, naomba
unikopeshe hizi pesa zako". Padri alipomuona
Teja akajibanza nyuma ya sanamu la Maria
pembeni na la Yesu. Teja akaendelea kueleza
shida zake halafu akainama na kuanza
kuchota michango. Padri kuona vile akatoa
sauti "Wewe acha hizoo". Teja aliposikia sauti
akajibu:
"Samahani Maria, nadili na mwanao sio wewe!
Na hizi sio pesa zakoo!"

No comments:

Post a Comment