Wednesday, March 28, 2012

Teh teh teh, CHUKUA HII...

Teh teh teh, CHUKUA HII...

Bubba aliingia offisini leo asubuhi macho yake yote mawili yakiwa mekunduuu yamevimba!!

Bosi akamuuliza, 
"Vp Bubba?!? Kulikoni??"

Bubba kajibu..
"Jana J'pili nlipokuwa kanisani mbele yangu alikaa mmama mmoja mneneeeeeeeeh, sasa tuliposimama wakati wa kuimba nyimbo za sifa, nligundua gauni lake limenasa kwenye makalio yake (MFEREJINI)... Kwahiyo nilipoona hivyo nikaamua kiroho safi kumsaidia kulichomoa!!! Ile namaliza kulichomoa makalioni mwake tuu, akanitwanga bonge la ngumi jicho la kulia..."

Bosi akauliza tena....
"Mbona sasa na la kushoto ni jekundu tena limevimba zaidi??"

Bubba akajibu kwa huruma....
"Yani we acha tuuu... Sasa mimi nlipoona hakupenda nilichomfanya si ndo nikaamua kulirudishia ndani kati kati ya makalio yake (MFEREJINI) kama lilivyokuwa..."

No comments:

Post a Comment