Mzungu alipanda ndege na
mbongo. Akaanza kumdharau na kuona hajui
kitu. Akamwambia mbongo "Tucheze mchezo
wakuulizana maswali. Ukiwa hujui unanipa
mimi dola 500 na nikikosa mimi nakupa
$10,000." kwa tamaa kwamba yeye mjuzi wa
yote. mbongo akasema sawa. Mzungu
akamuuliza, "nani walipigana world war I?".
Mbongo akawa hajui akamlipa mzungu $500.
Sasa mbongo akamuuliza mzungu," Kitu gani
kinaenda juu na miguu mitatu na kinarudi
chini na miguu minne?" Mzungu kimyyyaaa!
Akamplipa mbongo $10,000. Sasa
akamuuliza, "Haya sasa niambie jibu lake
nini?"
Mbongo akamrudishie $500, akamwambia
"sijui"
No comments:
Post a Comment