Wednesday, March 28, 2012

Pedeshe mmoja

Pedeshe mmoja akiwa na mkewe walikwenda muziki, binti mzuri alipita na kumsalimu pedeshe. kuona hivyo mama akapatwa shaka, basi yakaanza mahojiano:

Mama: Yule ni nani?’
Pedeshee: ‘Huyo ni nyumba ndogo yangu’.
Mama: Nataka talaka yangu’.
... Pedeshe: ’Powa nitakupa, lakini kumbuka safari za kwenda Uchina na Dubai ndio zitakuwa basi tena, na ishu za kwenda saluni mara mbili kwa wiki utazikosa, sijui utakuwa unatumia gari gani maana sitakuachia gari hata moja’.
Mama: kimya.

Basi mara akapita binti mwingine ikaanza awamu nyingine ya mazungumzo
Pedeshe: Mama watoto huyo aliyepita punde ni nyumba ndogo ya rafiki yangu’.
Mama: Mhhh huyu wala siyo mzuri kama nyumba ndogo yetu’

No comments:

Post a Comment